JINSI
YA KUIPATA SIMU YAKO YA YENYE OS (OPERATING SYSTEM) YA ANDROID ILIYOPOTEA AU
KUIBIWA
Habari ndugu
msomaji.Katika mfulululizo wa mada zetu leo nakuletea ujanja flani wa jinsi ya
kuipata simu yako iliyopotea,ibiwa au umeisahau mahali fulani!
Cha kufanya ni kuingia kwenye mtandao wa https://www.androidlost.com.Hakikisha
una akaunti ya gmail ili uweze kuingia. Ukifanikiwa, Ishushe application katika
play store inayoitwa Android lost kisha isanikishe katika kifaa chako. Hapo utakuwa umefikia nusu ya jinsi ya
kuitrak smartfoni iliyoibiwa au umesahau mahali ilipo kwa kutumia PC au simu
nyingine yenye interneti….
Kinachotakiwa hapa ni uwe na computer/simu
nyingine ambayo utaitumia kujua simu yako iko wapi.
Vifuatavyo ni vitu ambavyo utaweza
kuvifanya kwa kutumia mtandao wa Android lost.com!
§ Kuipiga simu
yako na itaita kwa kutumia computer yako au simu nyingine
§ Kujua mahali
simu yako ipo kwa kutumia google map katika computer/simu kwa GPS
§ kupata idadi
ya simu zilizopigwa baada ya kuibiwa
§ kupata sms
za mwisho kutumwa katika hiyo simu kama mtu aliyeiba kama bado anaitumia
§ kuifanya
simu yako itetemeke na kuipta kama umesahau sehemu uliyoweka
§ Kumtumia
message mtu aliyeichukua akurudishie na message hiyo itakua inatoka kama pop up
juu ya screen ya simu
§ Unaweza pia
kuificha App hiyo ili mtu asiweze kuiona na kuiondoa kwenye simu endapo
ameiba!!!!
Pia unaweza
kumpiga picha mtu aliyeishika hiyo simu hapo hapo na kujua ni nani!! Ni kweli
kama huamini comment hapo chini kwa email yako nikupe ujanja zaidi!!!
Cha muhimu
hapa ndugu msomaji ni kuwa na google account na uhakikishe simu yako imekua
installed na App hiyo baada ya kuipakua kutoka play store!
Pia unaweza kuitumia kujua mtu fulani anaongea
na nani sana lakini hapa mpaka upate account yake na password zake za gmail
kitu ambacho sii rahisi sana ila inawezekana kama wewe ni mbishi!
HUO HAPO JUU
NI MUONEKANO WA MTANDAO AMBAO UTAKUA UNAUTUMIA KUFANYA MAMBO YOTE HAYO
CHA MUHIMU NI KUCHAGUA UNACHOTAKA KUFANYA!!! KUNA MAMBO MENGI ZAIDI YA HAYO
AMBAYO UNAWEZA JIFUNZA CHA MUHIMU NI KUJARIBU KWANZA ILI UJIFUNZE MENGINE!!!
Ipakue hapa uanze kupata haya maujanja https://play.google.com/store/apps/details?id=com.androidlost
Maoni
Chapisha Maoni