HATUA KABLA YA MWANZO WA KOMPYUTA (1642)
Msomi mmoja kutoka Ufaransa aliyekuwa anaitwa Pascal, alianzisha
chombo cha kufanyia hesabu, ambacho alikitengeneza kwa ajili ya
kumsaidia baba yake katika kazi za hesabu, lakini hakikuwa na sifa bora
kama ilivyotakiwa. Kisha baada ya hapo kiliendelezwa na msomi mwengine
kutoka Ujerumani, ambaye alijulikana kwa jina la Lebnitz na kuzidishwa
ubora zaidi, kikawa kinafanya kazi zote za hesabu, kama vile kujumlisha,
kutoa, kugawanya na kuzidisha, badala ya kufanya kazi za kuzidisha na
kugawanya tu. Kisha msomi mwengine kutoka Uingereza alikuja kuanzisha
chombo chengine cha hesabu, ambacho kilikuwa na uwezo mkubwa wa
kuhifadhi vitu. Chombo hicho kilikuwa na sehemu kuu tatu, ambazo sehemu
ya kwanza ilikuwa ni kwa ajili ya kuhifadhia kumbukumbu, sehemu ya pili
ilikuwa ni kwa ajili ya kufanyia hesabu, na sehemu ya tatu na ya mwisho
ilikuwa ni kwa ajili ya kuchapishia.
 |
Pascaline first Calculator |
HATUA YA MWANZO (1944)
Kipindi cha mwaka 1944 kinajulikana kuwa ni
mwanzo
wa kudhihiri kompyuta. Kompyuta katika kipindi hicho ilikuwa ina sura
tofauti na hivi sasa, kwani ilikuwa ni kubwa mfano wa chumba, na ilikuwa
inatumika kwa ajili ya kufanyia hesabu tu, na ilikuwa inajulikana kwa
jina la (ENIAC) Electronic Numerical and Calculation. Na mwisho wa mwaka
1951 ilianzishwa kompyuta nyingine ambayo ilikuwa inaitwa Unifac, na
ilitengenezwa kwa ajili ya kufanyia biashara, na ilikuwa ni chombo pekee
ambacho kilikuwa na uwezo mkubwa wa kuhifadhi vitu.
HATUA YA PILI (1958)
Kipindi cha mwaka 1958 kilifanikiwa kuendeleza chombo cha kompyuta,
ambapo kilianzishwa chombo kinachoitwa Transistor, ambacho kiliwezesha
kutengeneza kompyuta yenye umbo dogo baada ya kuwa na umbo kubwa mfano
wa chumba. Vile vile chombo cha Transistor kiliwasaidia watumiaji wa
kompyuta kipindi hicho kuepukana na joto kali lililokuwa linatoka kwenye
kompyuta hiyo na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Na mwanzo wa miaka ya
sitini shirika la IBM lilianzisha chombo chengine cha kompyuta ambacho
kilikuwa na maendeleo zaidi katika kipindi hicho.
HATUA YA TATU (1964)
Kipindi hichi kilileta maendeleo makubwa sana katika kompyuta, ambapo
chombo cha kompyuta kilitengenezwa kwa kutumia (Integrated Circuits)
chombo hicho kilichukua nafasi ya Transistor. Na pamoja na maendeleo
makubwa kutokea mwaka 1972 shirika la
Intel
lilifanikiwa kutengeneza Processor ndogo ambayo ilibadilisha sura nzima
ya kompyuta katika umbo dogo sana (Mini Computer). Na hiyo ilikuwa ni
sifa pekee ya mabadiliko makubwa ya kompyuta, na katika kipindi cha
mwaka 1975 shirika la IBM lilianzisha kompyuta ya kutumiya mtu mmoja
(Personal Computer), vile vile katika kipindi hicho zilianzishwa
programu za kuendeshea vifaa vya kompyuta, na miongoni mwa programu hizo
ilikuwepo programu ya (Dos) Disk Operating System, Application
Programs, na programu za kutengeneza picha (Graphics).
HATUA YA NNE (1982)
Mwanzoni mwa miaka ya themanini kulianza kuenea matumizi ya kumputa zenye kutumia
Hard disk, na Processor zenye umbo dogo (Micro Processors) pamoja na programu za kuendeshea kompyuta (
Operating System). Pia zilianzishwa kopi za programu za kuendeshea kompyuta (Dos), na hapo ndipo ilikuwa mwanzo wa kutumia windozi (
Windows), na pia zilitumika programu nyingine ndani ya Windozi kama vile Word, Word 2, Word 6, Excel na power Point.
HATUA BAADA YA HATUA YA NNE (1995)
Kitu kinachosifika sana katika kipindi hichi ni kudhihiri kwa
programu za Windozi na kuwa kama ni mazingira pekee ya kuendeshea
kompyuta, na inajulikana wazi kwamba windozi ni kiini cha uendeshaji
katika kazi za kompyuta, na imeitwa windozi kwa sababu unaweza kuitumia
kufanyia kazi nyingi kwa wakati mmoja kwenye madilisha tofauti, kwa
mfano pale mtumiaji anapokuwa anasubiri windozi moja ifunguke anaweza
kuwa anasoma au kufanya kazi nyingine kwenye windozi nyingine pia.. Na
windozi ya kwanza kudhihiri ilikuwa ni Windows 95, 98, 2000, Millennium
kisha Windows XP, vili vile zilianzishwa programu maalumu kutoka kwenye
shirika la Microsoft, kama vile Microsoft
Office 97, Microsoft Office 2000 na Microsoft Office 2003, ambazo ambazo zinakusanya ndani yake
Microsoft Word,
Excel,
Access na Power Point, pia zinajulikana kwa jina la application
programs. Kisha kiliendelezwa kifaa cha Processor kutoka Pentium kwenda
Pentium 2, Pentium 3 na Pentium 4, pamoja na kuzidi uwepesi wa kufikia
vitu mpaka Giga Byte 2. Pia ilizidishwa nafasi ya kuhifadhia data ndani
ya Hard disk kiasi cha kufikia Giga Byte 300, na kufikia nafasi ya Ram
zaidi ya Mega Byte 512.
Mbona umeishia njiani
JibuFuta