JINSI INJINI YA NDEGE AINA YA JET INAVYOFANYA KAZI (JET ENGENE)
~Bila shaka umewahi kujiuliza 'injini ya ndege za abiria inafanyaje
kazi?!' Na huenda hukupata majibu!
Ukiendelea kusoma,utapata jibu la swali hilo! Kwanza,hebu tuone sehemu za injini ya ndege.
~Zifuatazo ni sehemu kuu tano za injini ya ndege (Jet Engine)!
1.KIIGIZA-HEWA (Air inlet)
~Hii ni sehemu ya mbele kabisa ya injini ambayo inakusanya hewa na kuiingiza katika sehemu inayofuata (inayoitwa Engine Air compressor (Kigandamizi-hewa).
2.KIGANDAMIZI-HEWA (Engine Air Compressor).
Ukiendelea kusoma,utapata jibu la swali hilo! Kwanza,hebu tuone sehemu za injini ya ndege.
~Zifuatazo ni sehemu kuu tano za injini ya ndege (Jet Engine)!
1.KIIGIZA-HEWA (Air inlet)
~Hii ni sehemu ya mbele kabisa ya injini ambayo inakusanya hewa na kuiingiza katika sehemu inayofuata (inayoitwa Engine Air compressor (Kigandamizi-hewa).
2.KIGANDAMIZI-HEWA (Engine Air Compressor).
~Sehemu hii ina kazi ya kugandamiza hewa
iliyoingizwa na kiingizi--hewa. Hewa inapogandamizwa,pressure inaongezeka. Na
pressure inapoongezeka,spidi ya hewa hiyo huongezeka. Kwa hiyo sehemu hii,inafanya
kazi ya kuongeza mwendo-kasi wa hewa inayoingia kwenye injini ya ndege. Baada
ya kukamilisha kazi hiyo,kazi nyingine ni kuielekeza hewa hiyo kwenye sehemu ya
tatu ya injini ya ndege.
3.JIKO LA INJINI (COMBUSTION CHAMBER).
Hapa ndipo nguvu inayoendesha ndege
inatengenezwa. Ni sehemu ambayo hewa iliyo chini ya mgandamizo na mafuta
vinakutana.
Pia,kuna plagi za cheche (spark plugs) zinazochochea mchanganyiko huo wa mafuta na hewa na kuwasha moto mkubwa/gesi zilizo moto sana (zilizo katika chumba kidogo lakini).
Gesi hizo zilizo chini ya mgandamizo mkubwa,zinaelekezwa kwenye sehemu nyingine tena ya nne ambayo,huelekeza gesi hizo zilizo na pressure kwenye sehemu inaitwa Turbine.
Sehemu hii ina mapanga/vitu kama feni vinavyozunguka kwa kasi sana ili kuongeza spidi/mwendo-kasi wa gesi hizo za moto.
Sehemu hiyo inatuleta katika sehemu ya tano ya injini inayoitwa Nozzle.
4.NOZZLE.
~Hapa,gesi hiyo inayosafiri kwa kasi sana,inanyooshwa (directed) kwenda sehemu ya mwisho ya nijini ya ndege ambayo inapeleka gesi hizo za moto nje ya ndege kwa kasi kubwa sana.
5.EXHAUST.
~Hapa ndipo gesi hizo hutolewa nje kabisa ya injini ya ndege baada ya kupita sehenu zote nne za mwanzo!
Nilikuwa nauliza je..?? Engine inaingiza upepo wa pressure ngapi..? Kwa mda gani..? Na inakuwa kwenye ration gan saa inatoka nje ya engine kulinga na ratio iliyo ingia...??
JibuFutaJe ndege ikitua unakaa mda gani mpaka izimwe au haizimwi kabisa
JibuFutaDeogratius Athanas Kingu
Futa