JE UNATAKA KUTENGENEZA APPS ZA SIMU AINA ZOTE, UWEZE KUUZA NA KUJIPATIA PESA KUTOKA ANDROID!? SOMA UJUE NINI CHA KUFANYA
Kama ulikuwa
unafikiri kwamba itachukua muda kwa HTML5 kutumika zaidi kwenye mobile app basi
unajidanganya. Ukweli ni kwamba HTML5 imekubalika na wataalam wengi wa IT
duniani kote kama standard kutenegeneza mobile apps. Hii ni kwasababu HTML5
tayari ni web-based standard, tofauti na language nyingine. Application
programs nyingi zina uwezo wa kufanya kazi vizuri kwa kutumia browser ambayo
imeandikwa kwa kutumia HTML5.
Faida kubwa ya
kutumia HTML5 ni developer anaweza kutengeneza HTML5 app inayoweza kufanya kazi
kwenye simu yoyote ya mkononi yenye browser nzuri. Hii itaondoa lile tatizo
lililopo kwamba app iliyotengenezwa kwa ajili ya platform za simu kwa mfano
Android haiwezi kufanya kazi kwenye platform nyingine kwa mfano iOS. Kwa
kutumia HTML5 hili tatizo litakuwa halipo tena.
Hadi sasa Linkedln
na Pandora zimeshaipitisha HTML5 kama standard ya kutengeneza applications
zake. Miaka kadhaa iliyopita Steve Jobs wa Apple alitabiri kwamba HTML5 kuwa
standard ya web apps. Apple waliamua kuipa kisogo Adobe Flash kutoka kwenye platform ya iOS. Kwa sababu Adobe
Flash ni plug in application, kumekuwa na shida kwa wengi kutumia application
kama You Tube ambayo inatumia Adobe Flash. HTML5 imeondoa tatizo hili, huhitaji
tena Adobe Flash kwa sababu una uwezo wa kutumia video moj kwa moja.
Tatizo
linaloikwamisha HTML5 kwa sasa ni jinsi program hii itaweza kuuungana vizuri na
simu za mkononi zilivyotengenezwa ili kuhakikisha inatumia features zote
zilizopo. Hiiinahusiana na features kama kamera, global positioning system
(GPS), n.k. Ikumbukwe kwamba application za kawaida za simu zinahusiana vizuri
na software ya simu kama vile Android. Hii iniwezesha application hiyo kujenga
uhusiano na hardware yenyewe inayoiwezesha kutoa huduma mbali mbali kwa mfano
kujua mteja alipo, kutoa direction kwa kutumia ramani, n.k
Kuna mengi mazuri
ya HTML5 yanakuja hivyo usiisahau kwenye vitu unavyotakiwa kuvijua japo kidogo
Maoni
Chapisha Maoni