SIMU YENYE UWEZO WA KUPIMA MALERIA
Wataalam
katika Chuo Kikuu cha Carlifonia wamo katika harakati za kutengeneza chip
ambayo itawekwa kwenye simu na kuwa na uwezo ya kugundua vijidudu vya Malaria
kwenye mwili wa binadamu. Wanasayansi wawili wa Chuo hicho Peter Lilhoj na
Chih-Ming Ho tayari wameshapata ruhusa ya kutengeneza kifaa hicho kutoka kwenye
vyombo husika. Kifaa hicho kitakuwa kinatumika mara moja na kutupwa
(disposable) na hivyo bila ya shaka kitakuwa ni kifaa cha kuchomeka tu badala
ya kutengenezwa ndani ya simu. Kitakuwa kinafanana na kadi ya sim, kwa hiyo ni
watumaini yetu kuwa kitatumika kwenye nafasi ya kadi kwa maana ya kwamba
hakutakuwa na simu maalum yenye kufanya kazi hii, bali ni simu zote.
Wakati
wametuacha bado tukitafakari ni vipi simu itapima na kugundua kilichopo kwenye
damu, wataalam hao wameeleza kuwa lengo la mradi huu ni kurahisisha na
kusambaza upimaji na ugunduaji mapema wa maradhi haya ambayo mpaka sasa
yameshateketeza maisha wa watu wengi mno Duniani na hasa katika nchi zilizoko
Amerika ya Kusini, Afrika na Bara Hindi. Mradi huu unategemea kuanza kutumika
nchini Msumbiji katika maeneo ya vijijini mara tu baada ya kukamilika kwa
utengenezajiwa kifaa hichi. Bila shaka hii italeta faraja kubwa katika
kuigundua Malaria hata hivyo matibabu hayatabadilika. Chuo Kikuu cha Carlifonia
hakikuthibitisha ni lini kifaa hichi kitakuwa tayari kutumika.
Maoni
Chapisha Maoni