Kwa mara nyingine tena wataalam -katika mambo ya silaha za kivita za kisasa-wa Jamhuri ya Kiislaam ya Iran wanatoka na Ndege mpya ya kivita inayokwenda kwa jina hili:Qaher-313.
Ndege hii ya kivita imezinduliwa katika mnasaba wa siku 10 wa kusherehekea ushindi wa Mapinduzi ya Kiislaam ya Iran ya mwaka 1979.Rais Ahmed Najad wa Iran ya Kiislaam amesikika akisema kwamba:Ndege hii ya Kivita imetengenezwa na kudizainiwa na wataalaam wa hapa Iran.
Ndege hii ya kivita kama unavyoiona kwenye picha ina sifa za kipekee,na hizi ni baadhi ya sifa -kama walivyozitaja wataalam wenyewe-:
1-Inauwezo wa kwenda speed kali sana na kubomoabomoa kambi au vituo vya adui na kurudi.
2-Inaumbo la kipekee linalojifanana,hakuna ndege nyingine duniani yenye umbo au muundo kama huo,ni mundo wa kwanza na muonekana wa kwanza kutoka uliobuniwa na Jamhuri ya Kiislaam ya Iran.
3-Wakati wa operesheni za ngege hii ya kivita,adui atapata tabu sana maana imetengenezwa katika mfumo ambao haiwezi kunaswa katika rada,hivyo inaweza kumfuata adui na kumtwanga na kisha kurudi pasina adui kutambua wala kuona ndege iliyomshambulia.
4-Silaha za kivita(roketi) zinazobebwa na ndege hii,hazionekani tofauti na ndege zingine ambazo roketi huonekana chini ya ndege hizi za kivita.Lakini hii jinsi ilivyotengenezwa ikiwa juu huwezi kuona ni wapi roketi zake zilipo,ikitaka kushambulia ndio inafungua ile sehemu ilikoficha roketi zake,na kuachia balaa kwa aduia.
5-Inapokwenda kutekeleza operesheni zake za kivita,basi inaonekana harakati zake katika chumba cha uongozaji (ardhini),na imepandikizwa ndani yake mfumo imara unaoiwezesha kugundua ndege za adui zikiwa angani na kwa mbali,kiasi kwamba adui mwenye ndege ya kivita anapokuwa angani na akiwa bado yuko mbali,ndege hii inakuwa nyepesi kumnasa na kumuweka katika target nzuri na hatimae kumsalimia.
Rais Ahmed Najad amesema:Maendeleo ya Iran katika sekta ya Kijeshi,hayana lengo la kuzivamia nchi nyinginezo na kuzionena ikiwemo kuzivunjia heshima kama vile kuzikalia kwa mabavu,bali ni maendeleo yanayolenga kulinda mipaka ya Jamhuri ya Kiislaam ya Iran,kulinda haki,amani na uhuru wa wanyonge.Na ni ishara au ujumbe wa upendo na urafiki kwa wote wapenda haki,amani na utulivu duniani.

Maoni
Chapisha Maoni