1. Kioo
Simu ya 2014
iwe na kioo chenye pikseli za hali ya juu, hii huleta ng’aro mzuri na pia
muonekano wa video na oicha huwa ni wa kuvutia, ni matarajio kuwa simu
walau ifikie piksel 400 kwa kila inchi (400 ppi), simu kadhaa zimefika na
kupita kiwango hichi zikiwemo simu kama vile Samsung Galaxy S5, HTC M8 na LG
G2, iPhone 5S kwa upande mwengine ina piksel 326 kwa kila inchi, pia na
Galaxy Note 3 nayo ina 386 ppi. Hivyo hizi ziko chini ya kiwango 400 ppi.
Ukubwa wa kioo pia ni suala muhimu kwenye simu. Ukubwa upi ni sahihi hutegemea
zaidi utashi binafsi wa mtumiaji. Sisi katika Gajetek tunaamini inchi 5 ni kioo
kilicho na ukubwa wa kiasi cha kutosha kwa ajili ya kuitumia simu kwa urahisi
huku kukiwa na ukubwa wa kutosha kuangalia media kama vile video za Youtube.
Kamera ni
sehemu ambayo kampuni zinazotengeneza simu zinafanya ushindani wa hali ya juu.
Wengi hudhani uzuri wa kamera ni wingi wa pikseli lakini ukweli ni kwamba kamwe
hilo sio sahihi. Kwa mfano ni vipi lenzi ya kamera ya simu inaweza kukusanya
mwanga wakati unapiga picha katika sehemu ambayo haina mwangaza mzuri, vile
vile kasi ya kamera ku-focus na hivyo kutoa picha zilizo nzuri (sharp). Nokia
wamejipatia sifa nzuri kwa upande wa kamera, hata hivyo simu ambazo zimetamba
kwa ubora wa kamera ni Sony Xperia Z2 na hata Samsung Galaxy S5. Na simu
ambayo kamera yake sio ya kuridhisha ni HTC One M8. Sio tu ina
megapikseli 4 (au kama HTC wanavyoiita Ultrapikseli) lakini mara nyingi kamera
hii hupoteza uhalisi wa rangi unapopiga picha, si ajabu kwa kamera ya simu hii
kajikuta una picha yenye mawingu ya pinki.
Vile vile kuna mambo ambayo yameingizwa kwenye
kamera lakini hayana umuhimu, au ni teknolojia iliyotangulia wakati,
mfano ni wachache ambao tayari wana TV za 4K lakini kuna simu kadhaa kama vile
Sony Xperia Z2, Samsung Galaxy S5 na Note 3 zinauwezo wa kuchukua video
za 4K wakati display za simu hizo hazionyeshi kiwango cha 4K. Hivyo tunadhani
hii ni ziada isiyo na faida kubwa kwa wengi miongoni mwa watumiaji.
Vifaa (accessories) ni ongezo muhimu katika simu. iPhone
ni simu inayoongoza kwa kuwa na vifaa vingi mbali mbali na vyenye matumizi
mazuri. Hata hivyo kifaa muhimu kabisa kwa sasa ni ama band za mazoezi za kuvaa
mkononi au smartwatch. Ingawa iPhone ina watengezaji binafsi wa saa au bandi
ambazo zinafanya kazi na iPhone, saa kama vile Pebble watch na band kama vile
Nike Fuelband, bado Apple wana haja kubwa kutoa saa yao binafsi. Samsung
kwa upande wa saa ndio kampuni inayooneka kuongoza baada ya kuwa na band moja
na saa tatu mpaka sasa hivi, Band ni Smsung Gear Fit na smartwatch ni Galaxy
Gear, Gear 2 na Gear 2 Neo. Ingawa bado hizi zinaonekana kuwa na
upungufu,wanachoonekana Samsung kuwatangulia wengine ni kuwa saa na bad hizi
zinafanya kazi za smartwatch na fitness band zote tatu. Kampuni kama vile LG na
Sony zote zimeshatoa ama band au smartwatch, ingawa bado hizi zinaonekana kuwa
ngeni katika medani hii.
Nguvu ya betri ndio lalamiko kubwa kwa watumiaji
wa simu. Nyingi kati ya simu hazifikisha hata siku kamili bila ya kuhitaji
kuchajiwa tena, na hasa kwa watumiaji wa hali ya juu (heavy users)
Tunaweza kusema teknolojia ya betri za simu bado iko nyuma mno kuweza kutoa
nguvu ya kutosha kwa watumiaji wa hali ya juu (heavy users) walau kuimaliza
siku nzima bila ya kuchaji. Kila ya simu inavyozidi kuwa na display kubwa
pamoja na pikseli nyingi basi nido kadiri simu unavyokula betri haraka.
Simu ambao inaonekana kuwa na unafuu mkubwa ni LG
G2 ambayo majaribio yameonyesha inaweza kudumu zaidi ya masaa 13 ni LG G2, simu
hii ina betri yenye nguvu kaisi cha 3000 mAh, ambapo simu kama vile Samsung Galaxy
S5, HTC M8 na Sony Xperia Z2 zote zina betri yenye nguvu ya 2500 mAh. Phablet
zenye vioo vya hali ya juu ndio zionaonekana kufanya vibaya zaidi kwenye suala
la chaja.
Betri ya hali ya chini ni ya iPhone 5S ambayo ina
mAh 1560. Pamoja na udogo huu bado betri hii haifanyi vibaya sana kulinganisha
na simu nyingine kwa vile iPhone ina display ndogo yenye pikseli chache
kulinganisha na simu nyingine za hali ya juu. Hata hivyo simu za mwaka 2014
zimekuja na mbinu ya kuzuia matumizi ya betri kwa mfano Samsung ina “Ultra Power
Saving Mode” ambapo simu inapowekwa katika mode hii inaweza ikadumu siku
kadhaa bila ya kuhitaji kuchajiwa, taarifa rasmi ya Samsung ni kuwa Betri
hudumu siku 12 bila ya kuchajiwa simu inapokuwa kwenye mode hii. Sony
Xperia Z2 nayo ina “stamina mode”.
Kila baada ya muda OS huboreshwa. Simu ambazo
zinafanya vizuri kwa kuboreshwa kwa muda mferu ni iPhone, una uhakika wa simu
yako kupata toleo jipya la OS kwa muda wa miaka mitatu au zaidi unapotumia
iPhone. KWa upande wa simu za Android Nexus peke yake ndio hupata
uboreshwaji kwa haraka na kwa miaka mingi. Simu zilizobaki kila tole jipya la
Android linapotoka basi kwa huchelewa na wao kuweka kwenye simu za wateja wao
lakini pia nyingi huwa hazipewi matoleo mapya ya OS baada ya miaka miwli.
Maoni
Chapisha Maoni