Kampuni
ya Microsoft katika hali isiyo ya kawaida imeamua kushirikiana na
wachakachuaji wa Windows Phone 7 na kuwafanya Sony na Apple
kuonekana kama kwamba si wenye busara. Makundi ya Jailbreakers au hackers wa
Windows Phone wanaojiita ChevronWP7 na Redmond wameruhusiwa rasmi na Microsoft
kuingiza apps na mambo mengine ambayo awali yalikuwa yakitumika kupitia mlango
nyuma tu katika Windows Phone 7, walifanya hivyo kwa vile walikuwa
hawatambuliwi rasmi na Microsoft. Makundi haya yanapenda zaidi kutambulika kama
Homebrew Communities (Jamii za watengeneza apps na waendelezaji wa OS binafsi)
kuliko hackers. Homebrew Communities hubadili firmware (OS), hutengeza apps na
kufungua (unlocking) gajeti hizo. Pia huwa na tabia za kutumia API ambazo
haziruhusiwi na hivyo kuwapa nafasi kufanya mambo ambayo developers watiifu
hawawezi kuyafanya.
Apple katika
vifaa vya iOS yaani iPad, iPod Touch, iPhone na Apple TV wamekuwa wakicheza
mchezo kufukuzana wa paka na panya na Makundi haya ya homebrew developers au
jailbrekers, baada ya Apple kushindwa mahakamani kufanya kuwa jailbreaking ni
kinyume cha sheria. Makundi mbali mbali ya hackers na developers kupitia Cydia
na masoko mengine yamekuwa yakijailbreak gajeti hizo na kuingiza apps zao
wenyewe. Hata hivyo kila pale ambapo Apple wamekuwa wakiboresha Firmware zao
(OS) wamekuwa wakizifunga tena gajeti hizo na hivyo kuwafanya wachakachuaji hao
kutafuta njia nyingine ya ku-jailbreak. Mchezo huu pia umekuwa ukiendelea baina
ya hackers na kampuni ya Sony katika Playstation 3 na PSP.
Hatua hii inaelekea kwamba Microsoft wamekubaliana
na hackers hawa kwa lengo la kuua uuzaji na ugawaji bure wa apps
kwa makundi hayo, kwani baada ya makubaliano haya kwa sasa Apps za Redmond na
ChevronWP7 zitakuwa zinauzwa. Hivyo Microsoft wataweza kupata hisa fulani
katika mapato ya hackers hawa. Hii ni njiia ya busara zadi ya vita dhidi ya
hackers badala ya kujaribu kutowatambua na kushindana nao jambo ambalo si Apple
au Sony wala hackers wanaonekana kupata ushindi.
Wakati kwa upande wa Microsoft huu unaelekea kuwa ni ushindi mkubwa
dhidi ya wachakachuaji, kwa upande wa wachakachuaji huu unaonekana kuwa ni usaliti
dhidi yao kwani muda si mrefu Chevron na Redmond watalazimika kuwa
watiifu kwa Microsoft, hivyo hawatatofautiana na developers wa kawaida. Lakini
je wachakachuaji wote watakuabaliana na Microsoft? Ni muda tu ndio utakaojibu
suali hili, lakini pia tukumbuke kwamba pesa inaweza kumtoa raisi ikulu.
Faida
kubwa inayopatikana kwa watumiaji wa kawaida katika Jailbreaking ni kupata
apps, themes na vitu kama hivi ambayo huwezi kuvipata kwenye Appstore ya Apple
na kwa upande wa Playstation humuwezesha mtumiaji kuingiza DVD za game ambazo
ni copy. Hasara kubwa ni kuwa kila mara inakubidi kujailbreak upya kifaa
chako na pia mara nyingi vifaa venye kuwanyiwa jailbreak hupoteza uimara au
utulivu (stability) wa OS. Na kwa upande wa Sony imekuwa ikiwafungia kucheza
online wale wote wenye kuchakachua kwenye Playstation zao.
|
The 23 Best Places To Bet On Casinos - Mapyro
JibuFuta› 2021/10/30 › The-23-best-places-to-bet-on-casinos- 동해 출장샵 › 2021/10/30 › The-23-best-places-to-bet-on-casinos- Nov 30, 2021 — Nov 30, 2021 The 23 당진 출장안마 Best Places To Bet On Casinos 나주 출장샵 · The 25 Best Places To Bet On Casinos 양주 출장안마 · 경기도 출장마사지 The 32 Best Places To Bet On Casino · The 43